Nawe, Nade2020-04-192020-04-192018Nawe, N. (2018). Taswira ya fisi katika ngano za Kiiraqw. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9578Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PJ2556.N382)Utafiti huu ulihusu taswira ya fisi katika ngano za jamii ya Wairaqw. Malengo mahususi yalikuwa: Kuchanganua taswira ya fisi inavyojitokeza katika ngano teule na, kueleza dhima ya taswira hizo katika jamii ya Wairaqw. Data za utafiti huu zilikusanywa katika mkoa wa Manyara wilayani Mbulu katika vijiji vya Titiwi na Landa. Kwa upande wa maktabani, data zilikusanywa katika Maktaba Kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Maktaba ya Dkt. Wilbert Chagula) na katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Mbulu. Data hizi zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano, ushuhudiaji, ukusanyaji wa matini na udurusu matini. Uchambuzi wa data umeongozwa na nadharia ya Semiotiki. Aidha, mkabala uliotumika kuchambua data hizo ni mkabala wa kitaamuli au maelezo. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba fisi ana taswira ya ujinga na upumbavu, tamaa na ulafi, umoja na mshikamano, woga na kukosa maamuzi sahihi, kukosa uwajibikaji na uvivu, maafa na mauaji na malezi mabaya. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa dhima za taswira ya fisi katika ngano za jamii ya Wairaqw ni kusaidia katika uhimizaji wa malezi ya watoto, uhamasishaji wa umoja na mshikamano, uzingativu wa ushauri mzuri na mbaya, uhamasishaji wa kufanya kazi kwa bidii. Pia, husaidia katika suala la kurithisha na kuendeleza mila na desturi ya jamii husika. Mbali na kushughulikia taswira ya fisi katika ngano za Kiiraqw, utafiti wa kina unahitajika katika ngano za jamii nyingine ili kubaini kama taswira ina dhima zinazofanana. Aidha, utafiti wa kina ufanywe kuhusu wahusika wengine wa kingano katika jamii ya Wairaqw na nyingine ili kutoa hitimisho la jumla.enIraqw languageCushitic languageTaswira ya fisi katika ngano za Kiiraqw.Thesis