Mwendamseke, Faraja Japhet2020-02-192020-02-192011Mwendamseke, F. J. (2011). Uanishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya Ki-bena. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/7222Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025T34M853)Utafiti huu unahusu uainishaji wa ngeli za nomino za lahaja ya Ki-Mwasamu ya lugha ya Ki-bena inayozungumzwa kusini magharibi mwa Tanzania katika wilaya ya njombe mkoani Iringa. Jumla ya watafitiwa 29 kutoka kata ya Imalinyi, lgima na Mdandu ndio waliohusika. uteuzi wao ulikuwa wa kinasibu. Taarifa zimekusanywa kwa watafitiwa kwa njia ya hojaji, mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu ulikuwa na malengo yafuatayo: kubainisha ngeli za Ki-Bena na idadi yake, kuchunguza mtawanyiko wa nomino zenye asili moja kisemantiki katika ngeli zilizoundwa kwa msingi wa kimofolojia na kufafanua dhima mbalimbali zinazojitokeza katika viambishi ngeli vya nomino. lli kutimiza malengo haya mikabala mitatu ya kinadharia imetumika ambayo ni: mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino, mkabala wa Viambishi vya Upatanisho wa Kisarufi na mkabala wa Kisemantiki. Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino umetumika kubainisha viambishi ngeli vya nomino katika misingi ya umoja na wings. Aidha mkabala wa Viambishi vya Upatanisho wa Kisarutl umetuinika pia kutokana na nomlno zmgine kutokuwa na viambishi dhahiri vya urnojzt na wingi. Katika uchunguzi wetu tumebaini kuna ngeli za Ki-Bona 18. Mkabala wa Kisemantiki umetumika kuchunguza mtawanyiko wa nomino zenye asili moja kisemantiki katika ngeli za msingi wa kimofolojia. Imebainika mtawanyiko wa nomino katika lugha ya Ki-bena upo katika nomino za viungo vya mwili, matunda, na wanyama. Mtawanyiko kama huu haupo katika nomino zinazohusu binadamu. Hivyo inatofautiana sana na lugha kami vile Kiswahili. Pia utafiti huu umebaini katika- lugha ya Ki-Bena, viambishi ngeli vya nomino vina dhima kama vile umoja/wingi, ukubwa/udogo na uzuri/ubaya. Dhima zote hizi huweza kujitokeza katika kiambishi kwa wakati mmoja na kusababisha utata. Pia kuna upekee unaojitokcza katika dhitna ya uzuri na ubaya ambapo dhima ya ubaya hutumika kwa binadamu na viumbe wanaufungwa na binadamu tu, lakini dhima ya uzuri ni kwa wote.otherBantu languagesNounsNjombe districtIringa regionUanishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya Ki-bena.Thesis