Mgallu, Amina2020-04-302020-04-302012Mgallu, A (2012) Mfungamano wa methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya wazigua, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaamhttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/10593Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,Japokuwa methali ni kipera kimojawapo kati ya vipera kadhaa vya fasihi simulizi kinachotumika katika maisha ya kila siku katika jamii, bado nafasi ya methali katika kuielewa mandhari na mazingira ya jamii inayotumia methali hizo haijatambuliwa na haijafanyiwa uchunguzi wa kina. Ili kubaini mfungamano wa methali na mazingira zinamotumiwa methali hizo, Tasinifu hii imejikita katika kutaflti juu ya mfungamano wa Methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya Wazigua. Methali zilizotumika katika utafiti huu zimetoka wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. Malengo ya utafiti huu ni kutambulisha maana zinazopatikana katika methali za Kizigua, kubainisha shughuli za kiuchumi za Wazigua zinazojitokeza kupitia maana za methali hizo na kutathimini mfungamano uliopo baina ya shughuli hizo za kiuchumi na methali za jamii ya Wazigua. Kwa kutumia mbinu na nyenzo kadhaa katika kukusanya na kuchambua data kama vile kompyuta, kinasa sauti, kinyonyi, kalamu na shajara, malengo hayo yamefikiwa na kukidhi haja ya utafiti. Vilevile utafiti ulitumia mbinu za uwandani kama vile mahojiano na ushiriki, pia mbinu ya maktabani ambayo ni uchambuzi matini. Mbali na mbinu hizi mtafiti aliongozwa na nadharia ya Sosholojia kwa kuzingatia mwelekeo wa Rondon (1968) na kwa kutumia mkabala wa kitaamuli au mkabala wa maelezo katika kubaini mfungamano wa methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya Wazigua. Kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa methali za Kizigua zinayasawiri mazingira ya jamii hii ya Kizigua.swwaziguaLanguage acquisitionSwahili languageSwahili literatureMfungamano wa methali na shughuli za kiuchumi katika jamii ya waziguaThesis