Venance, Furaha2020-04-072020-04-072017Venance, F. (2017) Dhamira za kisiasa katika mashairi ya bongo hip hop na jinsi zinavyoakisi jamii uchambuzi wa mashairi ya Joseph Mbilinyi (Sugu) na Ibrahimu Musa (Roma). Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.http://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9156Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8704.V462)Utafiti huu unachunguza dhamira za kisiasa katika mashairi ya Bongo Hip Hop na uakisi wake katika jamii, kutoka katika mashairi ya wasanii Joseph Mbilinyi (Sugu) na Ibrahim Musa (Roma). Mitazamo tofauti katika jamii juu ya muziki huu ndiyo iliyomsukuma mtafiti kufanya utafiti huu ili kuionesha jamii kuwa mashairi ya Bongo Hip Hop si upuuzi au uhuni bali ni fasihi komavu yenye dhima muhimu kisanaa na kijamii. Malengo mahususi ya utafiti huu yakiwa ni kubainisha namna mitindo ya lugha inavyosaidia kuibua dhamira za kisiasa, kubainisha dhamira za kisiasa zinazojitokeza na kuchambua namna dhamira hizo zinavyoakisi hali halisi ya jamii ya Kitanzania. Nadharia ya Sosholojia ya Fasihi na Mkabala wa Kitaamuli ndiyo uliotumika katika uwasilishaji na uchambuzi wa data. Mbinu za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni kusikiliza sidii za nyimbo za wasanii teule na udurusu wa machapisho mbalimbali yanayohusiana na mada husika. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa mashairi ya Bongo Hip Hop yamesheheni mitindo mbalimbali ya lugha inayosaidia kuibua dhamira za kisiasa. Mitindo hiyo ni tamathali za semi (kama vile tashibiha, sitiari, kejeli na tashihisi), misemo, misimu, takriri, ishara, na mgotanisho. Kwa upande wa dhamira matokeo ya utafiti yamebaini kuwa kuna dhamira za kisiasa zinazojitokeza katika mashairi ya Bongo Hip Hop ambazo kwa kiasi kikubwa zinaakisi hali halisi ya jamii ya Kitanzania. Dhamira hizo zinazoakisi jamii ni kama vile rushwa, ufisadi na umaskini, elimu, matabaka na ukosefu wa haki, tatizo la uongozi na uhuru wa kuzungumza na kutoa maoni. Utafiti huu umetoa mapendekezo mbalimbali ambayo yameelezwa vizuri katika sura ya tano.enSwahili poetryJoseph Mbilinyi (Sugu)Ibrahimu Musa (Roma)Dhamira za kisiasa katika mashairi ya bongo hip hop na jinsi zinavyoakisi jamii uchambuzi wa mashairi ya Joseph Mbilinyi (Sugu) na Ibrahimu Musa (Roma)Thesis