Habibu, Nasra2019-06-222020-01-072019-06-222020-01-072011Habibu, N. (2011) Muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya kisambaa. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available athttp://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspxhttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3398Available in printUtafiti huu, unachunguza muundo wa Kirai Kitenzi katika lugha ya Kisambaa. Mtafiti anachunguza ni vipashio gani vinaandamana na vitenzi katika sentensi za Kisambaa. Uchunguzi huu wa Kirai Kitenzi cha Kisambaa umefanyika kwa kutumia nadharia ya Sarufi Jumuishi ya Miundo Virai. Nadharia hii ni mojawapo ya nadharia za Sarufi Miundo Virai, zinazotumika kuelezea sintaksia ya lugha. Ni nadharia iliyoanzishwa na Gerald Gazdar mwaka 1970. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kitenzi cha Kisambaa kinaweza kisifuatiwe na kipashio chochote au kinaweza kuandamana na vipashio mbalimbali kama vile Kirai Nomino, Kitenzi kisaidizi, sentensi, Kirai Kielezi na Kirai Kihusishi. Hivyo Kirai Kitenzi cha Kisambaa kinaundwa na Kitenzi kimoja; Kitenzi na Kirai Nomino chenye nomino moja au mbili; Vitenzi viwili; Kitenzi na Kiunganishi tegemezi na Sentensi; Kitenzi, Kirai Nomino, Kiunganishi tegemezi na Sentensi; Kitenzi na Kirai Kihusishi; Kitenzi na Kirai Kielezi. Pamoja na hayo vilevile katika utafiti huu imebainika kuwa dhana ya uelekezi wa vitenzi inajitokeza pia katika vitenzi vya Kisambaa. Hii ni kwa sababu kuna Virai Vitenzi vinavyoundwa na kitenzi pamoja na Kirai Nomino chenye nomino moja ama mbili, pia vitenzi ambavyo si lazima viandamane na nomino bali vipashio vingine kama kielezi.enShambala languageMuundo wa kirai kitenzi katika lugha ya kisambaaThesis