Jeromin, Salome2021-04-302021-04-302016Jeromin, Salome (2016) Ujazilshaji Wa Kitenzi Katika Lugha Ya Kiswahili, Master dissertation, University of Dar es Salaamhttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/15187Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8702J47)Utafiti huu una lengo la kuchunguza uzalishaji wa kitenzi katika lugha ya Kiswahili. Kuna baadhi ya vitenzi vya lugha ya Kiswahili ambavyo vikatumika katika sentensi havikidhi mawasiliano, yaani havijitoshelezi kimaana. Vitenzi hivyo vinakuwa na maswali ya kujiuliza kama nini,nani na wapi. Hili lilikuwa tatizo lililohitaji kutafitiwa hasa kwa kubainisha vitenzi vinavtohitaji kukamilishwa na kufafanua kanuni na taratibu za ujazilishaji kimofosintaksia pamoja na kuibua changamoto za uzalishaji huo. Utafiti ulifanyika maktabani na baadae data zilikusanywa uwandani katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Stefano Moshi, Tanzania. Data ilikusanywa kwa njia ya mahojiano, hojaji, kusoma kamusi pamoja na mbinu ya kujichunguza. Ili kufanikisha kazi hii, nadharia ya Sarufi Geuza Mambo Zalishi iliongoza utafiti huu. Kazi hii imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeeleza kiini ncha utafiti na utaratibu uliozingatiwa katika kufanikisha utafiti. Sura ya pili imeshugulikia mapitio ya machapisho kuhusiana na ujazilishaji wa kitenzi katika lugha yay a Kiswahili. Mapitio haya yamebainishwakuwa kuna vitenzi vinavyohitaji kuamilishwa na vijenzi vingine. Sura ya tatu imehusu mbinu za utafiti ambapo sampuli, usambulishaji pamoja na njia nne za ukusanyaji data zilbainishwa. Sura ya nne, imeshugulikia uchanganuzi na uwaslishaji wa data. Kw3a ujumla data, iliyopatikanaimechanganuliwa kwa nia ya maelezo na takwimu. Sura ya tano imeshughulikia matokeo, hitimisho, na tafiti fuatishi. Baada ya hatua hizo utafiti umebaini kuwa lugha ya Kiswahili ina vitenzi vinavyojikamilisha kimaana na vitenzi vingine vinahitaji kukamilishwa na vijenzi vingine. Aidha vitenzi vinavyohitaji kukamilishwa na vijenzi vingine vimegawanyika katika makundi tofauti tofauti. Kuna vitenzi vinavyohitaji kukamishwa na kirai nombo kimoja, kuna vitenzi vinavyohitaji kukamiliswa na virai nombo viwilina kuna vitenzi vinahitaji kukamilishwa na tungo yenye kitenzi ndani yake. Pamoja na makundi hayo tofauti lakini vitenzi vya Kiswahili vikinyambuliwa huchukua ruwaza mpya. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa vitenzi mbavyo havijajitosheleza kimaana katika lugha ya Kiswahili vinakuwa na swali la kujiuliza. Vitenzi hvyo vinakamilishwa na vijenzi ambavyo vinajibu swali moja au maswali mawili kati ya maswali matatu; nini,nani na wapi. Katika lugha ya Kiswahili vitenzi vinapotumika katika sentensi vinaweza kuwa na maswali sawa ya kujiuliza lakini vijenzi vinavyotumika kujibu maswali hayo vikatofautiana. Baada ya kuwasilisha na kuchambua matokeo ya utafiti, tumejadili na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike zaidi juu ya mapendekezo hayo.enSwahili languageVerbsUjazilshaji Wa Kitenzi Katika Lugha Ya KiswahiliThesis