Mweta, Samweli Emmanuel2021-11-172021-11-172019Mweta S.E(2019)Matumizi ya nyimbo za watoto katika muziki wa bongo fleva,Masters dissertation,University of Dar es Salaam, Dar es Salaamhttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/16481Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF M1993.T34M83)Utafiti huu unahusu dhima ya matumizi ya nyombo za watoto katika muziki wa bongo fleva. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni;kubainisha nyimbo za muziki wa bongo fleva zinatotumia nyimbo za watoto, kubainisha dhamira zinazotokana na maatumizi ya nyimbo za watoto katika muziki wa bongo fleva , na dhima za matumizi ya nyimbo katika muziki wa bongo fleva . utafiti huu ulifanyika katika jiji la Dar es salaam katika wilaya tatu ambazo ni ilala, kinondoni na temeke, utafiti huu ulipitia maandiko mbalimbali hasa yanayohusu muziki wa bongo fleva na nyimbo za watoto. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingiliano matini na nadharia ya mwitiko wa msomaji/msikilizaji.misingi ya nadharia hizi ndiyo iliyosababisha katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti huu.utafiti huu ulifanyika maktabani na uwandni na ulitumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa data kama vile ukusanyaje nausomaji wa matini, kusikiliza na kutazama video za muziki wa bongo fleva ,na kufanya mahojiano.matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, muziki wa bongo fleva una matumizi ya nyimbo za watoto. Mtafiti amebaini kuwa nyimbo za muziki wa bongo fleva zinazotumia nyimbo za watoto ni pamoja na Mama wa MR.Nice, Hello wa Diamond na Dede wa Aslay kwa kutaja chache.Aidha , dhamira zinazotokana na matumizi yz nyimbo za watoto katika muziki wa bongo fleva ni mgawanyo wa majukumu katika familia, uvumilivu, mapenzi ya dhati na kufichua uovu katika jamii. Aidha kwa upande mwingine dhima za matumizi ya nyimbo hizo ni kuasilisha muziki wa bongo fleva kufanya wimbo/muziki kuwa maarufu, utambulisho wa jamii, kufikisha ujumbe kwa njia ya kitoto, kuleta mvuto katika muziki, kuhifadhi fasihi simulizi na kuleta majaribio katika bongo fleva. Aidha , nyimbo hizi zinatumiwa na wasanii wa muziki wa bongo fleva kutokana na umuhimu wake katika jamii. Nyimbo za watoto katika jamii hutunza historia ya jamii, huleta ushirikiano na yanaonesha kuwa muziki huu ni sehemu ya maisha ya jamii kwa kuwa yanayozungumziwa ni yale yanayotoka katika jamii husikaswChildren songMusicBongo flevaMatumizi ya nyimbo za watoto katika muziki wa bongo flevaThesis