Protection of refugees’ right to work in the east african community

dc.contributor.authorKatono, Evelyn Happy
dc.date.accessioned2020-06-10T20:50:24Z
dc.date.available2020-06-10T20:50:24Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF KZ6530.A353.K376)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza kiwango ambacho wakimbizi hulindwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Shabaha kuu ilikuwa kuchunguza ulinzi wa haki ya wakimbizi kufanya kazi, ambayo inaelezwa kuwa ni ya msingi sana kwa utu na uhai wao, na ni mhimili wa haki zingine zote. Hivyo, utafiti ulichunguza sheria za Jumuiya ya Afrika Mashariki kisha kuchambua kiwango ambacho zinalinda haki za wakimbizi kufanya kazi. Utafiti ulichambua sheria za kazi za nchi pamoja na sheria za wakimbizi za Kenya, Tanzania, na Uganda, ambazo ni nchi kuu tatu za Jumuiya zinazowahifahi wakimbizi wengi. Utafiti huu umerejelea mienendo bora kuhusu wakimbizi katika nchi na jumuiya zingine za kikanda kama vile Jumuiya ya Kiuchumi Afrika Magharibi (ECOWAS) na Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC), ambazo zina mifumo jumuishi hususani ya muingiliano wa wafanyakazi, ambao ni wakimbizi, jambo ambalo halipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ingawa kuna sheria za kuwalinda wakimbizi, hakuna ufanano katika ngazi ya Jumuiya, jambo linalochangia ukiukaji wa haki za wakimbizi. Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatumia sera-zuizi zinazolenga kulinda masoko ya ajira kwa raia wake. Wakimbizi wanahifadhiwa kwenye makambi bila kuwa na haki ya kutoka nje ya makambi hayo, hususani nchini Kenya na Tanzania, na hivyo kuathiri uhuru wao wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hata hivyo, Uganda inatekeleza mifumo ya makazi ya wakimbizi, ambayo ni huria zaidi na inayotoa matarajio mazuri zaidi kwa wakimbizi ya kushiriki katika kazi na uhuru wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine; ingawa mifumo hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa kutokana na sehemu yalipo makazi hayo. Utafiti huu umegundua kuwa misaada wanayopewa wakimbizi ni ya kiutu zaidi na kuna jitihada finyu za kuwapa misaada ya kimaendeleo, ambayo ingekuwa na tija kubwa katika upatikanaji wa ajira. Mikabala ya kilimwengu ya hivi karibuni kama vile Kiunzi cha Uhudumiaji Jumuishi wa Wakimbizi kinakosa utashi wa kisiasa wa mataifa na hivyo hakiwezi kuzaa matunda yaliyokusudiwa.en_US
dc.identifier.citationKatono, E.H (2019) Protection of refugees’ right to work in the east african community, Doctoral dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/12329
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectcommunityen_US
dc.subjectProtectionen_US
dc.titleProtection of refugees’ right to work in the east african communityen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
KZ6530.A353.K376.pdf
Size:
61.99 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections