Ujamaa vijijini

Date

1967

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali

Abstract

Jamaa ya kiafrika ya zamani iliishi kwa misingi ambayo sasa tunaiita misingi ya ujamaa.Ungewauliza wanaishiije,wasingekujibu kisiasa kama tunavyojibu sasa kwamba wanaishi kijamaa.Waliishi tu kijamaa na wala hawakujua namna nyingine ya kuishi.Waliishi pamoja na kufanya kazi pamoja kwa sababu hivyo ndivyo walivyoweza kusaidiana kupambana na matatizo mbali mbali ya maisha-mvua na jua,maradhi,hatari za wanyama au binadamu wengine,na safari nzima ya tangu kuanza maisha mpaka kufikia mauti. Matunda ya kufanya kazi pamoja hayakuwa yakigawanywa sawa sawa kabisa ,lakini sheria za kugawanya zilijulikana na msingi wake ulikuwa ni kwamba kila mmoja wa jamaa ana haki ya kupata chakula cha kutosha,mavazi ya kutosha,na mahali pa kulala kabla mtu mwingine(hata mkubwa wa jamaa) hajapta zaidi ya hapo.Walijiona kwamba ni kitu kimoja;na lugha zao na vitendo vyao vilisisitiza umoja wa jamaa yao.Mahitaji ya lazima ya maisha yalikuwa ni " chakula chetu","ardhi yetu","ngombe wetu".Hata namna ya kuitana ilisisitiza umoja na uhusiano wa ujamaa.Binti Fulani au Bin Fulani;Mama Fulani au Baba Fulani;Mka Fulani au hata mke mwenzi Fulani n.k Waliishi pamoja na kufanya kazi pamoja; na matunda ya kazi yao yalikuwa ni mali ya jamaa nzima.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class Mark ( EAF PAM HX451.T2A4)

Keywords

Socialism, Rural conditions, Tanzania

Citation

Nyerere,J.K (1967).Ujamaa vijijini. Dar es Salaam: Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali,p.33