Matumizi ya lugha na utambulisho wa jamii ya Wahaya waishio Dar es salaam

No Thumbnail Available
Date
2012
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu matumizi ya lugha na utambulisho wa jamii ya Wahaya waishio Dar es Salaam. Utafiti huu ulifanywa mkoa wa Dar es Salaam na kuhusisha Taasisi za elimu ya juu za Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Mzumbe kilichoko Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dar-es-Salaam. Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha lugha inayotumiwa zaidi na wazungumzaji wa jamii ya Wahaya wanapozungumza na Wahaya wenzao wakiwa Dar es Salaam katika maeneo ya nyumbani, majirani na kazini kwa kuzingatia kigezo cha umri na kubainisha nani anakubali/hakubali kujitambulisha na jamii ya Wahaya kwa kutumia lugha ya Kihaya. Jumla ya watafitiwa 60 walihusishwa katika utafiti huu. Watafitiwa hao walichaguliwa kwa kutumia sampuli nasibu tabakishi. Utafiti huu ulitumia mbinu za hojaji, mahojiano na ushuhudiaji katika mchakato wa ukusanyaji data. Utafiti huu umedhihirisha kuwa idadi kubwa ya watafitiwa wazee wanadumisha utambulisho wa Wahaya kwa kuendelea kutumia lugha ya Kihaya wanapowasiliana na wanajamii wenzao Wahaya waishio Dar es Salaam. Vilevile utafiti huu umebaini kuwa, watafitiwa wa rika la kati na vijana hawatumii Kihaya mara kwa mara wanapowasiliana na wanajamii wenzao Wahaya waishio Dar es Salaam. Watafitiwa wa rika la kati na vijana wanadumisha utambulisho wa Watanzania kwa kuendelea kutumia Kiswahili.
Description
Keywords
Haya language, Dar es Salaam
Citation
Theophil, P (2012) Matumizi ya lugha na utambulisho wa jamii ya Wahaya waishio Dar es salaam, Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)