Ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa kiswahili shule za sekondari mkoa wa Dar es salaam

Date

2012

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili katika shule za sekondari. Lengo ni kuchunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili tasinia ya ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili. Ili kufanikisha lengo hili, mtafiti alikusanya data kutoka shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Mbinu za utafiti za uwandani na maktabani zimetumika, mbinu za uwandani kama vile hojaji, usaili, kinasa sauti na ushuhudiaji, mtafiti alikusanya data mahususi zinazohusiana na utafiti. Tasinifu hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza, inahusu utangulizi wa jumla, sura ya pili mapitio ya maandishi, sura ya tatu mbinu za utafiti. Katika sura ya nne ni uwasilishaji, uchambuzi wa matokeo na mjadala, sura ya tano ni sura ya mwisho ambayo ni hitimisho na mapendekezo. Utafiti umebaini kwamba ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi hutumia mbinu na zana mbalimbali, mbinu hizo ni mbinu, zana shirikishi na zisizo shirikishi. Matokeo ya yanaonesha kwamba, walimu wanatumia sana mbinu na zana ambazo zisizo shirikishi kwa kuwa zinawapa fursa ya kumaliza mada mapema bila ya kujali wanafunzi wameelewa au la!. Utafiti unapendekeza kwamba tafiti maalimu zifanywe katika ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa kisasa, itasaidia kubainisha mbinu mbadala na bora za ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa kiswahili wa kisasa.

Description

Keywords

Swahili poetry, Secondary schools, Dar es Salaam region, Tanzania

Citation

Sultan, J. R