Mtazamo wa wasikilizaji wa redio kuhusu ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio: Mishano kutoka redio Ebony Fm na redio Country Fm katika manispaa ya Iringa
Loading...
Date
2016
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu kuchunguza mtazamo wa wasikilizaji wa redio kuhusu ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio hususan Redio Country FM na Redio Ebony FM. Utafiti huu umefanyika katika manispaa ya Iringa katika kata za Kitanzini, Gangilonga na Mkwawa. Utafiti huu ulikuwa na mlengo manne ambayo ni kubainisha ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio, kubainisha sababu zinowafanya watangazaji wa redio kubadili msimbo wakati wa utangazaji wa vipindi redioni, kuchunguza mtazamo wa wasikilizaji wa redio kuhusu ubadilishaji msimbo katika utangazji wa redio na kuonesha athari za ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio kwa wasikilizaji. Utafiti huu ulihusisha jumla ya watafitiwa 84 wakiwemo watangazji wanne kutoka katika vituo vya redio vilivyoteuliwa na wasikilizaji 80 kutoka kata tatu zilizoteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Mtazamo wa Wasikilizaji ya Bell mwaka 1984. Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji, hojaji na mahojiano. Aidha mikabala ya kimaelezo na kiidadi imetumika katika uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha ubadilishaji msimbo unaojitokeza katika utangazaji wa redio kuwa ni ubadilishaji msimbo ndani na ubadilishaji msimbo kati. Pia, matokeo yamedhihirisha kuwepo kwa sababu mbalimbali zinazowafanya watangazaji wa redio kubadili msimbo. Aidha, mtazamo wa wasikilizaji wa redio kuhusu ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio umedhihirtika kwa namna mbili, yani mtazamo chanya na mtazamo hasi. Vilevile, matokeo ya utafiti huu yameonesha athari chanya na athari hasi za ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio kwa wasikilizaji. Pamoja na matokeo hayo, imedhihirika kuwa mtindo wa ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio hutumika sana katika vipindi vya burudani.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library,(THS EAF PL8702.K521)
Keywords
Swahili language, Code switching (linguistics), Code mixing (Linguistics), Radio programs, Iringa region
Citation
Kididi, Z. S. (2016). Mtazamo wa wasikilizaji wa redio kuhusu ubadilishaji msimbo katika utangazaji wa redio: Mishano kutoka redio Ebony Fm na redio Country Fm katika manispaa ya Iringa, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.