Dhima ya semi zilizoandikwa katika daladala: uchambuzi wa Vipengele vya lugha na dhamira

Date

2011

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Slaam

Abstract

Semi ni tungo au kauli fupifupi za kisanaa zenye kubeba maana au mafunzo muhimu ya kijamii. Semi hutumia picha, tamathali na ishara. Aghalabu ni mafumbo yanayokusudiwa kubeba maudhui yenye maana zinazofuatana na ibara mbalimbali za matumizi. Kazi hii imechunguza dhima ya sema zilizoandikwa katika daladala katika jiji la Dar es Salaam. Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa ni kutafiti na kubainisha mitindo mbalimbali ya lugha na dhamira mbalimbali zinazojitokeza katika semi zilizoandikwa katika daladala. Ili kufanikisha utafiti huu, nadharia mbili zilitumika, Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji na Nadharia ya Sosholojia. Nadharia ya mwitiko wa msomaji ilitumika zaidi kwa makondakta, abiria, wapiga debe na wauza vitu mbalimbali waliokuwepo kwenye vituo vya daladala. Kwani, kila mtu alikuwa anatoa maana tofauti tofauti katika semi moja. Nadharia ya Sosholojia nayo ilitumika kwa sababu semi nyingi zilikuwa zikigusia masuala ya kijamii kama vile magonjwa ya UKIMWI, maadili na siasa. Mbinu za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji wa data katika kazi hii ni ushuhudiaji, maktaba na dodoso. Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data ni kamera, shajara na simu. Kwa jumla, matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha semi zilizosheheni mitindo ya lugha na dhamira mbalimbali. Pia matokeo hayo ya utafiti yalibainisha semi zilizoandikwa katika daladala zimeweza kuleta mchango mkubwa kwa jamii katika kuelimisha, kuburudisha, kuonya na kadhalika.

Description

Available in print

Keywords

Swahili literature, Daladala

Citation

Mturo, N. G. (2011) Dhima ya semi zilizoandikwa katika daladala: uchambuzi wa Vipengele vya lugha na dhamira. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx