Muundo wa virainomino katika Kitumbatu
No Thumbnail Available
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unalenga kubainisha muundo wa virainomino katika Kitumbatu kwa kutumia nadharia ya x̄ ambayo ni kifaa tumizi cha Sarufi Muundo Virai. Nadharia hii ilikuwa na lengo la kutoa maelezo ya kukibaini kirainomino cha lahaja hii kwa kuangalia vibainishi mbalimbali vinavyoifuata nomino na kwa kiasi gani nomino inavyoweza kutabiri utokeaji wa vibainishi kwa kuonesha kiwango cha mchomozo katika kirainomino cha Kitumbatu. Tasinifu hii ina sura sita. Sura ya Kwanza inatoa utangulizi wa jumla kwa kuelezea; usuli wa tatizo, tamko la tatizo la utafiti, malengo, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti na mpangilio wa utafiti. Sura ya Pili imeangalia mapitio ya machapisho pamoja na kiunzi cha nadharia kilichotumika kuchambulia data za utafiti huu. Aidha, Sura ya Tatu imeelezea mbinu za utafiti. Sura hii imebainisha mahali pa utafiti, watoataarifa, uteuzi wa sampuli, mbinu za ukusanyaji data ambazo zilikuwa ni mahojiano, hojaji na masimulizi. Pia uchanganuzi wa data, vifaa vya utafiti na mafanikio na upungufu wa utafiti. Sura ya Nne imejadili sifa za jumla za kiisimu za Kitumbatu. Sura ya Tano imejadili miundo ya virainomino vya Kitumbatu pamoja na vibainishi vyake. Na Sura ya Sita inatoa muhutasari wa utafiti, hitimisho na mapendekezo.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kirainomino cha Kitumbatu kina vibainishi tofauti kama vivumishi na viwakilishi. Kiwakilishi cha aina ya ‘kimilikishi’ kinaweza kutokea kabla au baada ya nomino. Vilevile kirainomino cha Kitumbatu kina mchomozo finyu na mchomozo mpana.
Description
Keywords
Swahili language, Tumbatu language, Zanzibar
Citation
Makame, K. O (2012) Muundo wa virai nomino katika Kitumbatu, Tasinifu ya M.A. kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx?)