Chimbuko na matumizi ya sinonimia katika kiswahili sanifu.

No Thumbnail Available
Date
2014
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia Chimbuko na Matumizi ya Sinonimia katika Kiswahili Sanifu. Malengo ya utafiti huu ni kuchunguza chimbuko na matumizi ya sinonimia katika Kiswahili Sanifu.Katika kufikia lengo kuu la utafiti huu, mbinu mbalimbali zilitumika. Mbinu hizo ni mapitio ya nyaraka mbalimbali, mbinu ya kujichunguza, mjadala katika makundi lengwa pamoja na mbinu ya hojaji. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni Nadharia ya Maana kama Matumizi ambayo huangalia namna watumiaji wa lugha wanavyoteua maneno kulingana na muktadha wa kimatumizi.Kuhusu matokeo ya utafiti imebainika kwamba umbali wa maeneo kijiografia, matabaka baina ya watumiaji wa lugha, wakati, mada, shughuli husika na hisia za mzungumzaji ni sababu za kuzuka na kumea kwa sinonimia katika lugha. Aina za sinonimi ambazo zimebainika kuwamo katika lugha ya Kiswahili Sanifu ni sinonimi nyepesi zinazofahamika kwa urahisi na wazungumzaji, na sinonimi kavu ambazo hazifahamiki kwa urahisi na wazungumzaji.Pamoja na hayo, utafiti umebaini faida kadha zinazopatikana kwa kuwapo sinonimia katika lugha, nazo ni fahari ya utambulisho bainifu kwa watumiaji wa lugha, kuwapo kwa wingi wa misamiati wenye kutoa wigo mpana wa uteuzi wa maneno katika lugha, kurahisisha mawasiliano, utambulisho kwa watumiaji wa lugha pamoja na fursa ya kulainisha ukali wa maneno. Halikadhalika tumebaini kuwa mifumo ya sinonimia katika matumizi ya sentensi ya Kiswahili Sanifu ipo yenye kulingana maana na kuna ambayo maana hazilingani.Kutokana na data zilizokusanywa kupitia utafiti huu tumebaini muktadha wa kimatumizi ndio chanzo kikuu cha chimbuko la sinonimia katika lugha. Utafiti huu unapendekeza kuwa, watumiaji wa lugha ya Kiswahili Sanifu wawe na uchaguzi wa maneno ya matumizi kulingana na muktadha husika wa mazungumzo.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.K4752)
Keywords
Swahili language, Synonyms and antonyms
Citation
Khamis, A, M(2014) Chimbuko na matumizi ya sinonimia katika kiswahili sanifu,Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.