PhD Theses
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing PhD Theses by Subject "Africa,"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uchambuzi linganishi wa Ujumi wa kifasihi katika simulizi teule za watumwa kutoka Afrika, Amerika na Ulaya.(Chuo Kikuu cha Dar es salaam, 2020) Henry, GUchambuzi linganishi wa Ujumi wa kifasihi katika simulizi teule za watumwa kutoka Afrika, Amerika na Ulaya. Grace Henry Tasnifu ya phD (Kiswahili) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, 2020 Utafiti huu unachambua kiulinganishi simulizi teule za watumwa kutoka Afrika, Amerika na ulaya ili kuonesha ujumi wa kifasihi unaojitokeza katika simulizi hizo. Aidha, licha ya madai yaliyopo kwamba simulizi za watumwa ni utanzu wenye nduni bainifu majumui, utafiti huu unajadili pia upekee wa simulizi za watumwa kutoka jamii hizo. Aidha licha ya madai yaliyopo kwamba simulizi za watumwa ni utanzu wenye nduni bainifu majumui, utafiti huu unajadili pia upekee wa simulizi za watumwa kutoka jamii hizo. Simulizi teule zilizochzmbuliwa ni Uhuru wa watumwa (1934) na Mama Meli: from Slavery to freedom (1993) kutoka Afrika: interesting narrative of the life of Frederick Douglass: an American slave (1845, na incidents in the life of a Slave Girl: written by Herself (1861) kutoka Amerika: na The letters of Ignatius Sanch. An African (1782) na History of Mary Price: a West Indian Slave (1831). Kutoka ulaya. Pia utafiti huu umechunguza mwingilianomatini uliopo kati ya simulizi za watumwa na kazi teule za fasihi ya Kiswahili ambazo ni tendehogo (1984) , kwaheri iselamagazi (1992), Miradi bubu ya wazalendo (1995) na kasri ya mwinyi fual (2007). Katika kukamilisha malengo ya utafiti huu, utafiti uliongozwa na nadharia za za Sosholojia ya kifasihi,, naratolojia, na mwingilianomatini. Mbinu mbalimbali kama vile eneo la utafiti, sampuli ya utafiti na usampulishaji zilitumika katika ukusanyaji, uhifadhi na uchambuzi wa data. Baada ya uchunguzi, ujumi wa kifasihi katika simulizi za watumwa kama vile msuko wa matukio, motifu, wahusika, na matumizi ya sauti na nafsi za usimulizi umejadiliwa. Aidha, umahususi wa ujumi wa kifasihi katika simulizi za watumwa kutoka jamii tofauti (afrika, Amerika Na Ulaya ) kama vile majina ya vitabu, baadhi ya ruwaza, na motifu umebainishwa. Umahususi huo unasababiswa na miktadha tofauti ya kihistoria, kiuchumi na kijamii iliyokuwapo katika jamii hizo kipindi cha utumwa na wakati wa utunzi wa simulizi husika. Baadhi ya miktadha hiyo ni jadi simulizi ya kiafrika, utawala wa Mwingereza, utangamano wa wa kijamii, mchango wa wanaharakati wa kikomesha utumwa na kadhalika. Pia, kama kazi za fasihi, simulizi za watumwa zinaingiliana na kazi nyingine za ubunifu za fasihi katika vipengele mbalimbali vya kifani na kimaudhui kama vile ruwaza, motifu, sauti za usimulizi, nafsi za usimulizi, na wahusika.