Browsing by Author "Sovu, Ahmad Yahya"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Matumizi ya Kiha katika kiswahili cha mazungumzo(University of Dar es Salaam, 2011) Sovu, Ahmad YahyaUtafiti huu unahusu matumizi ya Kiha katika Kiswahili cha mazungumzo uliofanywa katika manispaa ya Kigoma-Ujiji, mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Utafiti huu ulihusisha kata sita za Rusimbi, Kagera, Katubuka, Gungu, Bangwe na Kibirizi. Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha vipengele vya Kiha vinavyotumika katika Kiswahili cha mazungumzo; pili, kubainisha makundi ya jamii yanayotumia vipengele vya Kiha katika Kiswahili na kueleza sababu za kutumia vipengele hivyo; na tatu kueleza mchango wa Kiha katika Kiswahili. Jumla ya watafitiwa 96 walihusishwa na kuhojiwa katika utafiti huu. Watafitiwa hao walichaguliwa kwa kutumia sampuli nasibu tarbakishi. Katika mchakato wa ukusanyaji data utafiti huu ulitumia mbinu za hojaji , mahojiano, na ushuhudiaji. Utafiti huu umebaini kwamba wazungumzaji wa Kiha wanatumia vipengele mbalimbali vya kifonolojia vinavyotokana na sauti za Kiha katika Kiswahili cha mazungumzo. Vilevile, utafiti huu umebaini kwamba makundi ya watafitiwa yanayotumia sana vipengele vya Kiha ni wasiosoma shule, wakulima, wazee, wanawake, wafanyabiashara, na rika la kati. Sababu za makundi haya kutumia sana vipengele vya Kiha ni kwamba baadhi ya watafitiwa wana umahiri mkubwa wa kuzungumza lugha ya Kiha, na wengine hawakusoma shule, hivyo hushindwa kutofautisha matumizi ya Kiha na Kiswahili. Mwisho, utafiti huu umetoa mchango wa msamiati wa Kiha ambao unaweza kutumika katika Kiswahili.