Browsing by Author "Sehelele, Magdalena"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena.(University of Dar es Salaam, 2011) Sehelele, MagdalenaUtafiti huu unahusu mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena. Ingawa kuna tafiti zilizofanywa na Nurse (1979) na Priebusch (1935) kuhusu mfumo wa njeo na hali katika lugha hii, bado tafiti hizi zilikuwa za kiwango cha arabi na hivyo hazikufafanua kwa kina mfumo wa njeo na hali wa lugha ya Ki-bena. Utafiti huu ulilenga kuchunguza mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena hasa lahaja ya Ki-Lupembe kwa kuangalia ni vipengele vipi vya kimofolojia hubainisha njeo na hali. Pia, utafiti ulilenga kuchunguza mchango wa vielezi vya wakati na hali katika kubainisha muda na hali mahususi ya tukio katika sentensi yakinishi za Ki-bena. lli kutimiza malengo ya utafiti huu nadharia ya Ulalo iliyoasisiwa na Reichenbach (1947) ndiyo iliyotumika kuchambua data za ulafiti nadharia hii imefaa kutumiwa katika kuelezea mfumo wa njeo na hali katika lugha ya Ki-bena baada ya kufanyiwa marekebisho na wataalamu kama, Johnson (1977), Smith (1978) na Besha (1985). Data zilizotumiwa katika utafiti huu zilikusanywa kutoka katika vijiji vitatu vilivyopo katika tarafa ya Lupembe wilayani Njombe. Vijiji hivyo ni Kanikelele, Soliwaya na Lupembe Data za utafiti zilikusanywa kwa njia ya, mahojiano, dodoso na uchambuzi matini. Utafiti huu umebainisha kuwa katika lugha ya Ki-bena kuna mofimu sita (6) za njeo ambaza hujitokeza kabla ya mzizi wa kitenzi.Vile vile kuna mofimu nne (4) za hali ambapo mofimu tatu (3) hujitokeza baada ya mzizi wa kitenzi na mofimu moja (1) ambayo ni ya hali endelevu hujitokeza kabla ya mzizi wa kitenzi Utafiti huu pia umebainisha kuwa mofimu za njeo na hali hutumiwa pamoja na vielezi vya wakati na hali ili kubainisha muda na hali mahususi ya tukio.