Browsing by Author "Nnileka, Sharifa Mauridi"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Matumizi ya nadharia ya korasi katika uhakiki wa hadithi fupi: mifano kutoka mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine(University of Dar es Salaam, 2019) Nnileka, Sharifa MauridiUtafiti huu unahusu matumizi ya Nadharia ya 〖Korasi〗^1 katika uhakiki wa hadithi fupi: Mifano iliyotumiwa imetolewa kutoka Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni kubainisha vipengele vya Nadharia ya Korasi katika hadithi fupi mifano kutoka Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine. Kubainisha matumizi mbalimbali ya vipengele vya Nadharia ya Korasi katika hadithi fupi za Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine na kujadili umuhimu wa Nadharia ya Korasi katika uhakiki wa hadithi fupi. Utafiti huu ulipitia machapisho mbalimbali hasa yanayohusu uhakiki wa kazi za fasihi, hadithi fupi, Korasi na Nadharia ya Korasi. Korasi ni matendo, fikra au maneno ya kisanaa yanayojitokeza katika kazi ya sanaa ambayo humfanya msomaji au msikilizaji wa kazi ya sanaa kufikiria undani wa naneno, fikra au matendo hayo tofauti na kama maneno, fikra au matendo hayo yasingalijitokeza kwa namna yalivyojitokeza Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Korasi. Misingi na mihimili ya Nadharia ya Korasi iliwezesha kubaini matendo, maneno na fikra za kisanaa zinazojitokeza katika kila hadithi fupi kutoka Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine na hivyo kupata data za utafiti huu Aidha, mihimili ya Nadharia ya Korasi na hivyo kuzitafsiri kulingana na ujitokezaji wa korasi husika. Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo ukusanyaji wa data ulitumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa machapisho. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kwamba, Nadharia ya Korasi ni faafu katika uhakiki wa hadithi fupi. Katika hadithi fupi korasi imeweza kujitokeza kama tukio la kijamii, kama mhusika, kama sauti, kama kimya, kama ukengeushi, kama dhamira, kama muundo, kama mtindo, kama wimbo, kama imani, kama miviga na kama usimulizi. Umuhimu wa Nadharia ya Korasi uliobainika katika utafiti huu ni pamoja na kuwezesha kuchunguza ubunifu wa mwandishi, kuibua masuala ambayo hayajadiliwi kwa uwazi katika jamii, kukuza udadisi, kuondoa dhana ya kimapokeo inayoeleza kuwa kuhakiki fasihi ni lazima kutenganisha fani na maudhui, na kuhakiki matendo yasiyokuwa na maneno.