Repository logo
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
Repository logo
    Communities & Collections
    All of DSpace
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Ndumbaro, Eric Fortunatus"

Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya kulikoyela kahigi: uchunguzi wa mashairi ya kisasa (1973) na mageuzi (2015)
    (University of Dar es Salaam, 2017) Ndumbaro, Eric Fortunatus
    Utafiti huu umechunguza matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya Kulikoyela Kahigi ili kuona ufaafu wake katika jamii mamboleo na maendeleo ya ushairi andishi wa Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha vipengele vya kifani vya kingano kupitia mashairi ya Kahigi, kuchambua dhamira zinazoibuliwa kupitia vipengele vya kifani vya kingano pamoja na kujadili taathira za vipengele hivyo kwa ujumla. Data za utafiti huu zilikusanywa maktabani kutoka diwani za Mashairi ya Kisasa (1973) na Mageuzi (2015), pia kutoka katika maandiko mbalimbali. Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji ambapo mwandishi wa diwani teule alipewa na kuijaza. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na Kristeva (1980). Nadharia ya mwingilianomatini humakinikia uchangamani na mwingiliano uliopo baina ya matini moja na nyingine. Sambamba na hayo, mkabala wa kitaamuli ulitumika katika kuwasilisha na kuchambua data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa vipengele vya kifani vya kingano kupitia mashairi ya Kahigi ni pamoja na; takriri, baalagha, muundo, mianzo na miisho ya kifomula, onomatopea, wahusika, mandhari, mtindo wa usimulizi kama vile monologia, dialogia, fantasia, taharuki na nyimbo. Vipengele hivi vimesaidia kuibua dhamira mbalimbali kama vile uzalendo, harakati za ukombozi Afrika, umuhimu wa utamaduni asilia, umuhimu wa uvumilivu katika maisha, matabaka katika jamii, uovu na uonevu katika jamii, ujasiri na mafanikio pamoja na mapinduzi. Vilevile, imebainika kwamba vipengele vya kifani vya kingano katika mashairi ya Kahigi huibua na kubeba taathira anuwai. Miongoni mwa taathira hizo ni pamoja na kuleta upya na kuboresha mtindo wa uandishi wa mashairi, kutajirisha mtindo wa uandishi wa mashairi, kuondoa ukavu katika mashairi, kusawiri tabia na matendo ya jamii, kuhifadhi utamaduni asilia na kupanua mawanda ya miundo ya mashairi. Vilevile hupanua mawanda ya uhakiki wa mashairi, hubainisha maudhui ya mashairi husika, huongeza idadi ya hadhira, hukanganya hadhira pamoja na kusaidia kukwepa udhibiti. Kwa ujumla, matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa matumizi ya vipengele vya kifani vya kingano yameleta upya katika ushairi andishi wa Kiswahili. Inapendekezwa kuwa watafiti wengine wanaweza kuchunguza matumizi ya fani nyingine za kijadi katika mashairi ya watunzi wengine wa mkondo wa kimapokeo au wa kisasa ili kuweza kubaini maendeleo yaliyofikiwa katika ushairi andishi.

About Library

The University of Dar es Salaam Library is a vital source of scholarly information that facilitates users to get access to learning and research resources during their studies. It provides access to a wide range of resources in both print and digital formats and conducive reading environment for users, regardless of their physical conditions. All registered users are eligible to access library resources and can borrow print materials from general shelves for a specific period of time.

Useful Links

Koha Staff Login

University Research Repository

WebMail

Aris

Book Study Room

Mara Oral History

Hansard

SOCIAL MEDIA

Instagram

Facebook

Twitter

YouTube

WhatsApp

Ask Librarian

Contact Us

Postal Address
P.O.Box 35092
Dar es Salaam

Call Us: +255 22 2410500/9 Ext. 2165 ; Direct line +255 22 2410241

Fax No:: +255 22 2410241

Email:: directorlibrary@udsm.ac.tz

2025 University of Dar es Salaam - University Of Dar Es Salaam Library
Term of use / Privacy Policy