Browsing by Author "Mpalanzi, Lameck"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item An analysis of tense and aspect systems in Ikihehe: ‘A Case of Affirmative and Negative Constructions’(University of Dar es Salaam, 2010) Mpalanzi, LameckThis study examines the morphosyntactic properties of the Tense and Aspect systems (henceforth T/A) in Ikihehe. Although some scholars have sketchily discussed it, to date there is no sizable, detailed, typological or truly in-depth study of T/A in Ikihehe. In this endeavour, the study documents the morphological forms which mark T/A appearing in verbs in affirmative and negative constructions. In achieving the study objectives, two temporal theories were applied in the analysis, namely, Reinchebach’s linear model, which was supplemented by Guillaumean cognitive model. The primary data for this study was collected from Iringa district in Tanzania. The study relied much on synchronic observation, whereby information was collected through questionnaires, interviews, tape recording, text analysis and focus group discussions. The findings revealed that there are twelve (12) T/A formatives in Ikihehe, of which eight (8) are tense formatives which tend to occur in pre-root position and four (4) are aspect formatives, which occur in post-root, except for perfective and persistive markers. The findings also established that T/A markers tend to co-occur with specified aspectual adverbials. It has been observed that T/A are marked morphologically, tonologicaly and by periphrastic expressions. The findings further established that there are two negation markers si- and -laa- located in slot 1 and 5 on the verbal template. Moreover, the -si- negative marker tends to change the perfective markers from -é/ilé/ité/igé to negative suffixes -í/ilí/ití/igí. Although the study cannot claim to have solved the puzzles pertaining to the T/A systems in Ikihehe, it has laid the foundation for further exploration.Item Ujitokezaji wa falsafa ya Kiafrika katika Riwaya za kiethnografia za Kiswahili(University of Dar es Salaam, 2019) Mpalanzi, LameckUtafiti huu unachunguza ujitokezaji wa vipengele vya falsafa ya Kiafrika katika riwaya teule za kiethnografia za Kiswahili. Vipengele vilivyochunguzwa ni dini ya jadi, uganga na uchawi, uzazi, uhai na kifo na uduara wa maisha. Katika kuchunguza vipengele hivyo, riwaya zilizoteuliwa na kuchambuliwa ni Kurwa na Doto, Mirathi ya Hatari na Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka; Ntulanalwo na Bulihwali. Vilevile, utafiti ulilenga kubainisha namna vipengele teule vilivyomo katika riwaya vinavyoakisiwa katika jamii teule za Unguja, Njombe na Ukerewe. Aidha, utafiti ulilenga kuchunguza mwingiliano wa riwaya ya kiethnografia ya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika. Kadhalika, utafiti unafafanua mehango wa falsafa ya Kiafrika katika maendeleo ya fani na maudhui ya riwaya teule. Katika kukamilisha malengo haya, data ilikusanywa maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu ya udurusu wa maandiko maktabani, mahojiano, hojaji, ushuhudiaji na ushiriki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili kuanzia nyakati za ukusanyaji data hadi uchambuzi. Nadharia ya kwanza inaitwa Ontolojia ya Kibantu, na ya pili Sosholojia ya Fasihi. Ontolojia ya Kibantu ilituongoza kuchambua masuala yanayohusu falsafa yaKiafrika na Sosholojia ya Fasihi ilitusaidia kuhakiki masuala yanayohusu uhusiano wa fasihi na jamii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa fasihi hubeba falsafa ya jamii kwa kuwa vipengele teule vya falsafa ya Kiafrika vinadhihirika bayana katika riwaya teule. Utafiti umethibitisha kuwa tambiko linachukua sehemu kubwa ya dini ya jadi, ambayo ndiyo mzizi wa imani ya Waafrika. Jamii hizi zina matambiko mengi, mathalani, jamii ya Wamakunduchi ina tambiko is Mwaka-kogwa, tambiko la kumaliza msiba,tambiko la uzazi, tambiko la unyago na tambiko la mazishi. Jamii ya Wabena ina tambiko la kafara (Kipongo), Nyumbanitu na Amalimilo. Kwa upande mwingine, Wakerewe wana tambiko la kuzaliwa, uzazi na kutanabahi katika pembe, tambiko la kumtoa mtoto nje,tambiko la harusi, tambiko la kuvundika ndizi, tambiko la ugonjwa na tambiko la mazishi. Pia, Wakerewe, wana tambiko la machifu huko Kitare, tambiko katika makumbusho ya Handebezyo na katika "Jiwe Linalocheza." Utafiti umebaini kuwapo kwa imani mseto katika jamii teule inayotokana na mwingiliano wa dini ya jadi na dini za kigeni. Kuwapo kwa imani mseto ni jitihada za jamii teule kutafuta utambulisho na ukubalifu wa kila kundi. Utafiti umebaini kuwa upo mpaka bayana kati ya fani ya uganga na uchawi kwa kuzingatia kigezo cha utendaji, dhima, kiwango cha nguvu-hai, miiko na ufantasia wa fani hizo. Uchunguzi katika riwaya na jamii teule umebaini kuwapo kwa makundi kumi (10) ya waganga na makundi mawili (2) ya wachawi. Utafiti unaonesha kuwa baadhi ya waganga na wachawi wanaishi maisha duni kwa kuwa hutumia gharama kubwa kununua viambato vya uganga na uchawi. Licha ya kufumbata falsafa mbalimbali za maisha, suala la uzazi katika jamii ya Ukerewe ni mfano dhahiri wa kuwapo kwa familia pana ya Kiafrika inayojumuisha watu-hai, waft' na watakaozaliwa. Sanjari na hilo, utafiti huu unaafiki kuwa kifo kwa Mwafrika si mwisho wa maisha kwani mfu huendelea kuwapo kama inavyoelezwa katika Ontolojia ya Kibantu. Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa maisha ya maana na halisi ni ya hapa duniani. Aidha, utafiti huu ulibaini kuwapo kwa uhusiano wa kiduara kati ya mtu, jamii na mfumo uliopo. Kiontolojia, utafiti umethibitisha kuwapo uhusiano wa kiduara kati ya Mungu, mizimu, wahenga, binadamu, wanyama na mimea, na vitu na mahali. Katika kudhihirisha fasihi inavyobeba falsafa ya jamii, utafiti huu umetambua kuwa fasihi na falsafa ya Kiafrika hutenda majukumu yanayofungamana. Mwisho, utafiti huu unabainisha kuwa falsafa ya Kiafrika ni malighafi na nyenzo muhimu katika uandishi wa fani na maudhui ya riwaya ya Kiswahili.