Repository logo
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
Repository logo
    Communities & Collections
    All of DSpace
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Mollell, Rehema Dismas"

Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Dhima za mhusika mzimu katika riwaya teule za Kiswahili: uchunguzi wa Babu Alipofufuka (2001) na Marimba ya Majaliwa (2008)
    (University of Dar es Salaam, 2017) Mollell, Rehema Dismas
    Utafiti huu umechunguza dhima za mhusika mzimu katika riwaya teule za Kiswahili, uchunguzi wa Babu Alipofufuka na Marimba ya Majaliwa. Utafiti huu ulichochewa na mawazo ya baadhi ya wataalamu kuonesha kwamba, mizimu haina nafasi yoyote katika jamii ilihali wataalamu wengine wakionesha nafasi na umuhimu wa mizimu katika jamii. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka katika riwaya ya Babu Alipofufuka (Mohamed, 2001) na Marimba ya Majaliwa (Semzaba, 2008). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhalisiamazingaombwe pamoja na nadharia ya Ontolojia ya Kibantu. Nadharia ya Uhalisiamazingaombwe ilitumika katika lengo la kwanza lililohusu kubainisha sifa za mhusika mzimu katika riwaya teule za Kiswahili pamoja na lengo la pili ambalo lilikuwa ni kueleza namna mhusika mzimu alivyosawiriwa. Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu ilitumika katika lengo la tatu lililohusu kujadili dhima za mhusika mzimu katika riwaya zilizoteuliwa. Utafiti umebaini sifa mbalimbali zilizomtambulisha mhusika mzimu katika riwaya teule kama: kujitokeza kama ndoto, kufanya matendo ya ajabu, kutoa msaada, kutokeza kama sauti ya kicheko, kutokeza katika mazingira ya ajabu, kubadilika sura na umbo. Waandishi wamemsawiri mhusika mzimu akiwa na sifa hizi kwa lengo la kuonya, kuonesha ugumu wa maisha, kukemea ubadhilifu wa mali ya umma unaofanywa na viongozi, kukejeli utamaduni wa nje, kuonesha makazi ya mizimu na kuendana na mazingira aliyomo. Kwa upande mwingine, waandishi wamemsawiri mhusika mzimu kama mpinga ukoloni mamboleo hasa matumizi ya vitu visivyoendana na utamaduni wa Mwafrika kama vile matumizi ya lugha za kigeni kama Kiingereza. Aidha, mzimu amesawiriwa kama mpinga uongozi mbaya hususani viongozi wenye ubinafsi wa kujipendelea wenyewe pasipo kujali wananchi, dhuluma na matumizi ya mabavu kwa lengo la kuwagandamiza wanyonge. Vilevile, mzimu amesawiriwa kama mzalendo katika kuwakumbusha viongozi kutumikia wananchi waliowachagua, mwalimu katika kutoa historia ya matukio mbalimbali yaliyotokea zamani pamoja na utohoaji wa hadithi. Mzimu pia amesawiriwa kama mwenye kujiamini katika kukabiliana na vikwazo pamoja na kutoa msaada kwa wanyonge wanaodhulumiwa ili waweze kupata haki yao. Katika utafiti huu, dhima za mhusika mzimu zilizojitokeza katika riwaya teule ni pamoja na: kukamilisha dhana ya uduara katika kuonesha kwamba kuna kuwapo baada ya kifo, mzimu kama kiumbe cha usamehevu wa makosa kupitia mahusiano ya kidarajia na Mungu, kuonya kwa kukataza mambo yasiyoendana na jamii, kinga ya mabaya pamoja na kutambika.

About Library

The University of Dar es Salaam Library is a vital source of scholarly information that facilitates users to get access to learning and research resources during their studies. It provides access to a wide range of resources in both print and digital formats and conducive reading environment for users, regardless of their physical conditions. All registered users are eligible to access library resources and can borrow print materials from general shelves for a specific period of time.

Useful Links

Koha Staff Login

University Research Repository

WebMail

Aris

Book Study Room

Mara Oral History

Hansard

SOCIAL MEDIA

Instagram

Facebook

Twitter

YouTube

WhatsApp

Ask Librarian

Contact Us

Postal Address
P.O.Box 35092
Dar es Salaam

Call Us: +255 22 2410500/9 Ext. 2165 ; Direct line +255 22 2410241

Fax No:: +255 22 2410241

Email:: directorlibrary@udsm.ac.tz

2025 University of Dar es Salaam - University Of Dar Es Salaam Library
Term of use / Privacy Policy