Browsing by Author "Mlowezi, Dickson"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Lugha ya vijana wa dar es salaam na utambulisho wao: Mifano kutoka Kiswahili(University of Dar es Salaam, 2012) Mlowezi, DicksonUtafiti huu unahusu Lugha ya Vijana wa Dar es Salaam na utambulisho wao kwa kuzingatia mifano kutoka Kiswahili. Utafiti huu uliofanywa katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania. Utafiti huu ulihusisha manispaa tatu za Ilala, Kinondoni na Temeke ambapo kata moja kutoka kila manispaa iliteuliwa. Kata hizo ni kata ya Segerea iliyoko manispaa ya Ilala, kata ya Mwenge iliyoko manispaa ya Kinondoni na kata ya Mbagala iliyoko manispaa ya Temeke. Lengo la utafiti lilikuwa ni kubainisha muundo na matamshi ya msamiati na sentensi za Kiswahili zinazotumiwa na vijana wa Dar es Salaam katika kubainisha utambulisho wao na kueleza sababu zinazowafanya vijana hao watumie lugha hiyo. Jumla ya watafitiwa 76 (wanaume 45 na wanawake 31) kati ya watafitiwa 96 walishiriki katika utafiti huu. Katika mchakato wa ukusanyaji data, mtafiti alitumia mbinu za hojaji, mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu umedhihirisha kwamba vijana wa Dar es Salaam wana matamshi yao, msamiati wao, na sentensi zao ambazo huzitumia wakiwa katika mazungumzo yao. Vilevile utafiti huu umedhihirisha kuwa lugha ya vijana wa Dar es Salaam ina muundo wake wa matamshi, msamiati na sentensi ambapo kimsingi miundo hiyo inafuata mpangilio wa lugha ya Kiswahili. Mwisho, utafiti huu umebaini sababu mbalimbali za vijana wa Dar es Salaam za kutumia lugha ya Kiswahili kwa namna yao ya kipekee zikiwemo: kuficha maana iliyokusudiwa na vijana wenyewe, kuleta ucheshi na utani miongoni mwao, kuonesha mshikamano miongoni mwa vijana wenyewe, kuficha siri za vijana zisitoke nje ya vijana wenyewe na ni mazoea yaliyojengeka miongoni mwa vijana wenyewe.