Browsing by Author "Mbijima, Rose Jackson"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Dhima ya visasili katika jamii ya Wagogo.(University of Dar es Salaam, 2011) Mbijima, Rose JacksonVisasili ni utanzu mmojawapo wa fasihi simulizi unaopatikana katika jamii nyingi za Afrika na ulimwcngu kwa ujumla Visasili ni hadithi za kale zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe na namna na shabaha ya maisha yao. Utafiti huu unahusu uchunguzi wa visasili katika jamii ya Wagogo. Utafiti ulikuwa na malengo mawili, kubainisha visasili vya Kigogo na kuhakiki dhima ya visasili hivyo Katika kufanikisha malengo ya utafiti, nadharia ya kiuamilifu imetumika katika uchanganuzi wa data. Data ilikusanywa kutoka mkoa wa Dodoma. Mbinu ya mahojiano ilitumika katika zoezi la kukusanya data sambamba na matumizi ya hojaji na kanda zilizorekodiwa na walaalamu wengine kuhusu visasili na zile alizorekodi mtafiti wakati akiwa uwandani. Utaflti ulibaini visasili viwili katika jamii ya Wagogo, ambavyo ni kisasili cha "Wang'omvya rafiki wa simba" na kingine ni "Babu asiyekuwa na shukrani." Dhima za visasili zilizobainishwa kwa kuzingatia visasili viwili vilivyopatikana katika utafiti. Kama tanzu nyingine za fasihi simulizi, utanzu wa visasili una mchango mkubwa katika maisha ya kila siku ya mwana jamii. Huelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali hasa yale yaliyotokea zamani na yanayoaminika kuwa ni ya kweli na yanaeleza kuhusu asili ya mambo kadha wa kadha katika jamii Visasili huonesha utamaduni wa jamii husika hasa kupitia kwenye ibada za miviga na matambiko. Ni utanzu unaoturudisha nyuma kabisa kuona historia ya Mwafrika kabla ya kuja kwa wageni walioleta dini mpya kutukumbusha tulikuwa tunaabudu vipi, nani, wapi na kwa namna gani Visasili ni uwanda ambao unahitaji tafiti zaidi za kitaaluma kutokana na umuhimu wake na dhima yake katikajamii. Inapendekezwa kuwa tafiti zifanywe katika vipengele vingine vya lugha, na kadhalika. Aidha, tafiti linganishi zifanywe kwa jamii tofauti tofauLi zenye visasili. Utafiti kuhusu tanzu nyingine mbali na visasili pia unaweza kufanyika katika jamii ya Wagogo, kwa mfano, hadithi za ngano methali na nyinginezo.