Browsing by Author "Makosa, Baraka"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Matumizi ya kiswahiili na lugha nyingine katika utoaji wa huduma za afya mkoani Lindi(University of Dar es Salaam, 2013) Makosa, BarakaUtafiti huu wa Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na lugha nyingine katika utoaji wa huduma za afya ulifanyika katika wilaya ya Lindi na manispaa ya Lindi. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kubainisha nani anatumia Kiswahili na nani anatumia lugha nyingine katika utoaji wa huduma kwenye hospitali na zahanati, kubainisha maeneo yanayotumiwa zaidi na Kiswahili na maeneo yanayotumiwa zaidi na lugha nyingine na kujadili athari za matumizi ya lugha ya Kiswahili na lugha nyingine katika utoaji wa huduma kwa watumiaji na lugha zenyewe. Utafiti huu ulihusisha jumla ya watafitiwa 43. Mtafiti alikusanya data kwa kutumia mbinu za mahojiano na hojaji. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa makarani, wauguzi na wafamasia wanatumia zaidi Kiswahili wakati madaktari na wasanifu maabara wanatumia zaidi Kiingereza. Pia, wanawake wanatumia zaidi Kiswahili, huku wanaume wakitumia zaidi Kiingereza. Wazee na rika la kati wanatumia zaidi Kiswahili wakati vijana wanatumia zaidi Kiingereza. Vilevile, matokeo yameonesha kuwa maeneo yanayotumiwa zaidi na Kiswahili ni mapokezi, chumba cha madawa na wodini na maeneo yanayotumiwa zaidi na lugha ya Kiingereza ni chumbani kwa daktari na maabara wakati lugha za jamii hazitumiwi katika utoaji wa huduma. Baadhi ya athari zilizobainishwa ni kuwepo kwa tafsiri potofu ya maneno kutoka lugha za kigeni, kuwa na msamiati changamani wa Kiswahili na lugha nyingine, kwa kuzitaja chache. Kutokana na matokeo hayo, utafiti huu umependekeza kuwa Kiswahili kipewe kipaumbele katika utoaji wa huduma kwenye hospitali na zahanati ndipo lugha nyingine zifikiriwe kutumika. Katika utoaji wa huduma za kijamii, lugha zinazoeleweka kwa wanajamii wengi ndizo zitumike na kuwepo kwa juhudi za kuhakikisha kwamba Kiswahili kinatumiwa kwa kiwango kikubwa katika utoaji wa huduma katika hospitali na zahanati.