Browsing by Author "Machumi, Deo"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Matumizi ya maneno ya mitaani katika magazeti pendwa na matokeo yake katika kiswahili(University of Dar es Salaam, 2015) Machumi, DeoJamii ya Watanzania kwa kipindi kirefu imekuwa na mazoea kuwa habari zinazoandikwa au kutangazwa kupitia vyombo vya habari huzingatia matumizi ya Kiswahili rasmi. Lakini mara baada ya kuruhusiwa kuanzishwa vyombo vya habari binafsi, baadhi ya vyombo hivyo vilibadilisha kidogo matumizi ya lugha ambapo vilianza kutumia maneno ya mitaani katika uandishi wa habari. Matumizi hayo ya maneno ya mitaani katika vyombo vya habari yaliibua mjadala miongoni mwa wanajamii wazungumzaji wa Kiswahili huku baadhi yao wakianza kuhoji mustakabali wa lugha hiyo utakuwaje kwa siku zijazo. Hali hii ndiyo iliyotulazimu kuchunguza matokeo ya matumizi ya maneno ya mitaani katika magazeti pendwa katika Kiswahili. Utafiti huu umefanyika katika jiji la Dar es Salaam na wilaya ya Magu iliyo mkoa Mwanza. mbalimbali za ukusanyaji data zimetumika katika utafiti huu ambazoni hojaji, maktabani na usaili. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa baadhi ya maneno ya mitaani katika magazeti pendwa ni kitalu cha kukuzia msamiati wa Kiswahili. Mapendekezo mbalimbali yametolewa katika utafiti huu baadhi yakiwa; BAKITA na taasisi nyinginezo zinazojishughulisha na lugha ya Kiswahili kuielimisha jamii kuwa baadhi ya maneno sanifu ya Kiswahili chanzo chake ni maneno ya mitaani. Mwisho utafiti huu umetumia Nadharia ya “Mtazamo wa Hadhira” ya Bell (1984) kama mwongozo.