Browsing by Author "Li, Zhou"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Ulinganishaji wa taratibu za uainishaji wa maneno baina ya Kiswahili na Kichina cha kisasa.(University of Dar es Salaam, 2016) Li, ZhouUtafiti huu umechunguza taratibu za uainishaji wa maneno katika Kiswahili na Kichina cha kisasa. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa kufafanua taratibu za uainishaji wa maneno katika Kiswahili na Kichina pamoja na kulinganisha na kulinganua taratibu hizo kati ya lugha hizi mbili. Ili kufikia malengo hayo, utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Isimu-amilifu ya Kimfumo (Systemic Functional Linguistics/SFL). Kutokana na nadharia hiyo tumetambua kwamba maneno hujibainisha kwa kazi zinazofanywa na maneno hayo katika ngazi ya juu zaidi yaani virai, vishazi na sentensi. Mtafiti alitumia mbinu ya uchambuzi wa matini wakati wa ukusanyaji wa data ambazo zilipatikana maktabani. Zaidi ya hayo, alitumia mkabala wa kitaamuli. Katika utafiti wetu, tumepata matokeo ambayo yameonyesha ufanano na tofauti kadhaa zilizotokea wakati wa ulinganishaji wa taratibu za uainishaji wa maneno baina ya Kiswahili na Kichina. Katika lugha ya Kiswahili tumebaini kategoria tisa (9) za maneno wakati katika Kichina tumebaini kategoria kumi na nne (14). Aidha, tumetambua kategoria zote za Kiswahili zipo katika Kichina. Zaidi ya hayo, lugha zote mbili zimetumia vigezo vitatu vya kiisimu katika uainishaji wa maneno. Vigezo hivyo ni kigezo cha kisintaksia, kimofolojia na kisemantiki. Pamoja na hayo, tumebaini kwamba taratibu za uainishaji wa maneno katika Kiswahili zimeegemea zaidi katika kigezo cha kimofolojia wakati katika Kichina zimeegemea zaidi katika kigezo cha kisintaksia. Kwa kifupi tumegundua kwamba bado kuna mikanganyiko kadhaa katika uainishaji wa maneno ya lugha hizi mbili.