Repository logo
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
Repository logo
    Communities & Collections
    All of DSpace
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Kileo, Joan Godwin"

Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya kisiha
    (University of Dar es Salaam, 2017) Kileo, Joan Godwin
    Lengo la utafiti huu ni kuchunguza athari za Kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha. Utafiti huu una malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha maneno ya lugha ya Kiswahili yaliyomo katika lugha ya Kisiha, kueleza athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha, na kufafanua sababu za athari za kimofofonolojia za lugha ya Kiswahili katika lugha ya Kisiha. Chanzo cha data kilichotumika katika utafiti huu ni uwandani. Data zilikusanywa kwa njia ya mahojiano, hojaji na ushuhudiaji kutoka kwa wazee wenye rika la kati ya miaka 50-85 na wanafunzi wa kati ya miaka 10-14 katika wilaya ya Siha. Data zilizopatikana katika utafiti huu zilichambuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles (1982). Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa lugha ya Kisiha imeathiriwa na lugha ya Kiswahili hasa katika kipengele cha mofolojia. Aidha, athari za kifonolojia zimejitokeza katika kipengele cha sauti za Kiswahili zilizotumiwa na watoa taarifa wakati walipokuwa wanazungumza Kisiha. Athari hizo ni matumizi ya sauti [z] badala ya sauti [s], sauti [m] badala ya sauti [n], sauti [ch] badala ya sauti [sh] pamoja na udondoshaji wa sauti [h] ya Kisiha. Fauka ya hayo, utafiti huu umeweka bayana sababu za athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha, ambapo miongoni mwa sababu hizo ni elimu, biashara, pamoja na upanuzi wa matumizi ya Kiswahili vijijni. Mwisho ni muhtasari wa utafiti, matokeo ya utafiti, mchango wa utafiti pamoja na mapendekezo ya tafiti fuatishi ambapo imependekezwa kuwa tafiti zifanyike katika vipengele ambavyo havikushughulikiwa, kama vile sintaksia na semantiki. Aidha, kuna haja ya kufanya tafiti kuhusu mbinu na mikakati ya kuchochea matumizi ya lugha ya Kisiha katika muktadha huu wa kutamalaki kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kudumisha lugha ya Kisiha.

About Library

The University of Dar es Salaam Library is a vital source of scholarly information that facilitates users to get access to learning and research resources during their studies. It provides access to a wide range of resources in both print and digital formats and conducive reading environment for users, regardless of their physical conditions. All registered users are eligible to access library resources and can borrow print materials from general shelves for a specific period of time.

Useful Links

Koha Staff Login

University Research Repository

WebMail

Aris

Book Study Room

Mara Oral History

Hansard

SOCIAL MEDIA

Instagram

Facebook

Twitter

YouTube

WhatsApp

Ask Librarian

Contact Us

Postal Address
P.O.Box 35092
Dar es Salaam

Call Us: +255 22 2410500/9 Ext. 2165 ; Direct line +255 22 2410241

Fax No:: +255 22 2410241

Email:: directorlibrary@udsm.ac.tz

2025 University of Dar es Salaam - University Of Dar Es Salaam Library
Term of use / Privacy Policy