Browsing by Author "Kauti, Juma Mussa"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mabadiliko ya dhamira katika nyimbo za makuzi ya mwanamke wa kiyao(University of Dar es Salaam, 2013) Kauti, Juma MussaTasinifu hii ni matokeo ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Dhamira Katika Makuzi ya Mwanamke kupitia nyimbo za kabila la Wayao. Tasinifu imejadili mabadiliko ya dhamira katika nyimbo hizo kulingana na makuzi ya mwanamke katika hatua tatu za makuzi ya mwanamke yaani kuvunja ungo, ujauzito wa kwanza na uzazi wa kwanza. Tatizo la utafiti lilichagizwa na haja ya kubaini maisha, mazingira na mahusiano yamhusuyo mwanamke katika hatua hizo tatu za makuzi katika jamii. Lengo la utafiti lilikuwa ni kubainisha mabadiliko ya dhamira katika nyimbo za makuzi ya mwanamke, lililochagizwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kuchunguza dhamira za nyimbo za makuzi, kubainisha usawiri wa nyimbo katika makuzi na kuchopoa athari za nyimbo katika makuzi ya mwanamke. Katika kufikia malengo hayo, mtafiti alifanya utafiti wa nyaraka na uwandani na ametumia mbinu za hojaji, mahojiano, majadiliano, Data mbalimbali zilipatikana na kuchambuliwa kwa kufuata malengo ya utafiti. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, dhamira za nyimbo katika makuzi ya mwanamke hubadilika kulingana na makuzi ya mwanamke; hivyo kuleta usawiri katika maisha ya mwanamke katika jamii. Kwa mtazamo huo utafiti unadhihirisha kuwa mwanamke ana majukumu mengi yanayohitaji msaada kutoka kwa wanajamii wengine lakini kwa bahati mbaya mila zingine bado hazijatambua suala hili.Utafiti unapendekeza kwa kuiasa serikali na jamii kulinda na kuthamini utu wa mwanamke bila ya kukengeusha mila na desturi za jamii, hatua hii inakusudia kuboresha malezi na maadili ya jamii kwani kwa kufanya hivyo makuzi ya mwanamke yataweza kuboreka.