Browsing by Author "Jilala, Hadija"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item The artistic uses of metaphors in constructing meanings and messages in new generation songs in Tanzania(University of Dar es Salaam, 2008) Jilala, HadijaThis study is about the artistic use of metaphors in Kiswahili new generation songs in Tanzania. The purpose of i-investigating metaphors was to examine the artistic uses of metaphors in constructing meaning and messages in new generation songs. To realize its objectives, the study employed three methods of data collection: interviews, questionnaire and focused discussion groups. The research was conducted in Dar es Salaam. The researcher mainly used the cognitive theory of metaphor to identify, categorize and analyse metaphors and the meanings and messages they construct. The study found out that the artistic use of metaphors in new generation songs is a complex phenomenon which cannot be seen in isolation unless it combines with other stylistic devices such as metonym, allegory, similes, synecdoche, proverb, symbolism and slang in constructing meanings and messages. Therefore, the audience comprehends meaning of a metaphor on the basis of the context of use, body of knowledge and experience and socio-cultural relations. Furthermore, the study found that the suggestive meaning of metaphors gravitates around certain themes of society such as HIV/AIDS, gender inequality, role of woman, love and sexuality and socio-economy. This study therefore is anchored in stylistics as a discipline. It draws the attention the question of language use in new generation songs. It shows that meanings stylist artistically embodied in language devices such as metaphors. It is and messages are art expected that the insights from the study will help to deepen our understanding of the artistic uses of metaphors in constructing meaning and messages and thus promote our appreciation of metaphors as a driving force behind the attractiveness of new generation songs.Item Athari za kiutamaduni katika tafsiri mifano kutoka matini za Kitalii katika makumbusho za Tanzania(University of Dar es Salaam, 2014) Jilala, HadijaUtafiti huu umeshughulikia athari za kiutamaduni zijibainishazo katika tafsiri kwa kuchambua matini za kitalii zilizopo katika Makumbusho za Tanzania. Nia ya kufanya hivyo ni kuibua modeli ya kutafsiri matini za kiutamaduni ambayo itakuwa kiunzi cha kutafsiri matini za kiutamaduni ili kudhibiti mapungufu ya kimawasiliano. Dira iliyoongoza katika utengenezaji wa modeli ni matokeo ya utafiti huu na mhimili wa mawazo ya Nadharia ya Skopos. Ili kuibua Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni, tulitathmini mbinu za kutafsiri matini za kiutamaduni, mikakati iliyotumika katika uteuzi wa visawe vya kiutamaduni, mapungufu ya kimawasiliano yanayosababishwa na athari za kiutamaduni na namna tunavyoweza kukabiliana nayo. Data za utafiti huu zilipatikana kwa kutumia mbinu za usomaji wa machapisho, dodoso, usaili, uchunguzi shirikishi na upimaji. Utafiti huu umegundua kuwa, mbinu zinazotumika kutafsiri matini za kiutamaduni hazina uangavu na hivyo kusababisha mapungufu mengi ya kimawasiliano. Kichochezi kikuu cha mapungufu ya kimawasiliano ni mwachano wa kiutamaduni baina ya utamaduni chanzi na utamaduni lengwa. Ili kupunguza dosari hizo, utafiti huu umependekeza Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni (MMK) ambayo ni kiunzi cha kutafsiri matini za kiutamaduni ili kuleta ufanisi wa mawasiliano. Mhimili mkuu wa modeli hii ni fikra kwamba, ujumbe wa matini ya kiutamaduni ndiyo huukilia mbinu za tafsiri. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa mbinu inayofaa kutafsiri matini za kiutamaduni ni “uasilishaji na ufafanuzi wa visawe”. Mbinu hii ndiyo nguzo kuu ya Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni.