Repository logo
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
Repository logo
    Communities & Collections
    All of DSpace
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Hans, Mussa Mohamed"

Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Mchango wa lahaja katika kukuza na kuendeleza kiswahili sanifu hazina fiche iliyomo katika lahaja za kiswahili za Zanzibar
    (University of Dar es Salaam, 2014) Hans, Mussa Mohamed
    Utafiti huu ulikusudia kuchunguza msamiati unaohusu majina ya samaki wa baharini katika jamii ya wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili zilizoko Zanzibar. Lengo likiwa ni kubaini namna lahaja hizi zinavyoweza kuchangia katika kukuza na kuendeleza Kiswahili Sanifu. Hata hivyo, ilionekana kwamba litakuwa jambo la welekevu iwapo pia historia ya wazungumzaji wa lahaja hizo na mchango wao katika historia ya lugha ya Kiswahili vitachunguzwa kwa kina. Data za utafiti zilipatikana uwandani kwa kuhusisha mbinu mbalimbali ambazo ni ushuhudiaji, usaili, hojaji na majadiliano katika majopo. Baaadhi ya data pia zilipatikana maktabani. Kwa upande wa uchambuzi wa data, palitumika mbinu ya kikompyuta kuchambulia data za kimsamiati na data za kihistoria zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Mwachano - Makutano ya Lugha za Kibantu pamoja na nadhariatete ya Ndugu na Ndugu wa Mbali iliyoasisiwa na Massamba (2007). Nadharia hii pamoja na nadhariatete inayoishajihisha kwa kiasi kikubwa inawiana na matokeo ya utafiti. Hata hivyo, katika utafiti huu imependekezwa kwamba nadhariatete ya Ndugu na Ndugu wa Mbali ifanyiwe marekebisho kidogo kwa kuongezewa dhana ya Ndugu wa Karibu ili kuakisi vema uhusiano ulioko miongoni mwa lahaja za Kiswahili na pengine lugha mbalimbali za Kibantu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili kupitia katika lahaja zao wana mchango mkubwa sana katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili hususani katika uwanja wa msamiati unaohusu majina ya samaki wa baharini pamoja na uwanja wa historia ya lugha ya Kiswahili kwa ujumla. Utafiti kuhusu msamiati wa majina ya samaki wa baharini mbali na kutoa taarifa zinazohusu majina ya aina anuwai za samaki na sifa zao, umebainisha pia msamiati mpya ambao haumo katika Kiswahili Sanifu. Katika mjadala huu pia utafiti umeweka bayana tofauti ya kimsamiati baina ya Zanzibar na Tanzania bara, tofauti ambazo pia zinajitokeza katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyoandikwa na TUKI na Kamusi la Kiswahili Fasaha iliyoandikwa na BAKIZA. Hata hivyo imependekezwa kwamba utafiti mwingine katika jamii za wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili unaweza kuelekezwa katika msamiati unaohusu nyanja nyingine kama vile utamaduni na tiba. Katika utafiti wa kihistoria, mbali na mambo mengine utafiti umebainisha kwamba chimbuko la wazungumzaji wa lahaja za Kimakunduchi, Kitumbatu na Kipemba ni maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Kenya hususani maeneo yanayopatikana katika upwa wa Afrika Mashariki. Maeneo hayo ni pamoja na Bagamoyo, Tanga, Dar es Salaam, Mtwara na Mombasa. Hata hivyo, kuna baadhi ya watoa taarifa waliodai kwamba chimbuko lao ni Shiraz (Pashia) ingawa hawakuwa na ushahidi usiosailika.

About Library

The University of Dar es Salaam Library is a vital source of scholarly information that facilitates users to get access to learning and research resources during their studies. It provides access to a wide range of resources in both print and digital formats and conducive reading environment for users, regardless of their physical conditions. All registered users are eligible to access library resources and can borrow print materials from general shelves for a specific period of time.

Useful Links

Koha Staff Login

University Research Repository

WebMail

Aris

Book Study Room

Mara Oral History

Hansard

SOCIAL MEDIA

Instagram

Facebook

Twitter

YouTube

WhatsApp

Ask Librarian

Contact Us

Postal Address
P.O.Box 35092
Dar es Salaam

Call Us: +255 22 2410500/9 Ext. 2165 ; Direct line +255 22 2410241

Fax No:: +255 22 2410241

Email:: directorlibrary@udsm.ac.tz

2025 University of Dar es Salaam - University Of Dar Es Salaam Library
Term of use / Privacy Policy