Repository logo
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
Repository logo
    Communities & Collections
    All of DSpace
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Abdul, Atiba"

Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Maana na sababu za kiisimujamii kwenye majina ya koo za Kiluguru
    (The university of Dar es Salaam, 2013) Abdul, Atiba
    Utafiti huu ulihusu majina ya koo za jamii ya Waluguru ambao wanapatikana upande wa Mashariki mwa nchi ya Tanzania. Utafiti ulifanyika katika Wilaya ya Morogoro Vijijini kwa kuhusisha vijiji vitano ambavyo ni Rudewa, Kinole, Tegetero, Mkuyuni na Mifulu. Jumla ya watafitiwa arobaini walihusika katika kutoa taarifa zilizohusiana na mada ya utafiti . Watafitiwa hao waliteuliwa kwa kutumia njia mbili ambazo ni njia ya usampulishaji nasibu na njia ya usampulishaji tajwa. Kadhalika data ilikusanywa kutoka kwa watafitiwa kwa kutumia njia tatu ambazo ni njia ya usaili/ mahojiano, njia ya hojaji na njia ya ushiriki. Malengo ya utafiti huu yalikuwa mawili nayo ni kubaini Maana za Majina ya Koo za Kiluguru na kubaini Sababu za Kiisimujamii kwenye Majina ya Koo za Kiluguru. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni ya Makutano na Mwachano ya Giles ya mwaka 1982. Nadharia hii ilitumika ili kuonesha jinsi majina ya koo katika jamii ya Waluguru yanavyowiana na kutofautiana hususani katika kipengele cha maana na sababu za kiisimujamii kwenye majina ya koo hizo. Utafiti huu ulibaini kwamba, maana na sababu za kiisimujamii kwenye majina ya koo za Kiluguru huukiliwa na mambo mbalimbli yakiwemo majina ya wanyama, majina ya mimea,matukio yaliyojitokeza katika jamii, hali tabia za watu, mwonekano wa watu, majina ya makazi, ujuzi/shughuli za watu, majina ya vitu na majina ya makabila mengine. Pia utafiti ulibaini kwamba baadhi ya majina maana zake huwa katika mahusiano yaani uwepo wa jina moja hupelekea kuwepo kwa majina mengine. Vilevile utafiti ulibaini kwamba baadhi ya majina yalikuwa yakibadilika kutokana na matukio yaliyojitokeza katika koo husika na umbali wa kijiografia. Halikadhalika utafiti ulibaini kwamba majina ya koo katika jamii ya Waluguru yalikuwa yakitolewa kwa kuzingatia jinsi za wahusika. Mwisho utafiti ulibaini kwamba majina ya koo katika jamii ya Waluguru yapo katika kategoria nne za maneno ambazo ni nomino, vitenzi, vivumishi na vielezi.

About Library

The University of Dar es Salaam Library is a vital source of scholarly information that facilitates users to get access to learning and research resources during their studies. It provides access to a wide range of resources in both print and digital formats and conducive reading environment for users, regardless of their physical conditions. All registered users are eligible to access library resources and can borrow print materials from general shelves for a specific period of time.

Useful Links

Koha Staff Login

University Research Repository

WebMail

Aris

Book Study Room

Mara Oral History

Hansard

SOCIAL MEDIA

Instagram

Facebook

Twitter

YouTube

WhatsApp

Ask Librarian

Contact Us

Postal Address
P.O.Box 35092
Dar es Salaam

Call Us: +255 22 2410500/9 Ext. 2165 ; Direct line +255 22 2410241

Fax No:: +255 22 2410241

Email:: directorlibrary@udsm.ac.tz

2025 University of Dar es Salaam - University Of Dar Es Salaam Library
Term of use / Privacy Policy