Repository logo
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
Repository logo
    Communities & Collections
    All of DSpace
  • English
  • Català
  • ÄŒeÅ¡tina
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • LatvieÅ¡u
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Srpski (lat)
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Log In
    New user? Click here to register. Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Abdalah, Fatuma"

Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Uingizaji wa semi katika kamusi ya kiswahili sanifu (2013) Mifano kutoka katika Methali, Nahau na Misemo
    (University of Dar es Salaam, 2014) Abdalah, Fatuma
    Utafiti huu ulikusudia kuchunguza uingizaji wa semi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la Tatu la mwaka 2013. Lengo likiwa kubaini namna semi zilivyoingizwa, kubainisha upungufu uliojitokeza na kupendekeza mbinu za kukabiliana na upungufu huo. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika utafiti wa maktabani Toleo la Tatu la Kamusi ya Kiswahili Sanifu lilichunguzwa ili kubaini namna semi zilivyoingizwa. Utafiti wa maktabani pia ulijikita katika kuchunguza kazi za watafiti mbalimbali waliomakinikia Kamusi ya Kiswahili Sanifu ingawa kazi zao zilijikita katika matoleo ya nyuma ya kamusi hii. Katika utafiti wa uwandani mbinu za hojaji na usaili zilitumika wakati wa kukusanya data za utafiti huu. Data zilizopatikana zilichambuliwa kwa kutumia njia ya maelezo na njia ya kitakwimu. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Maana ni Matumizi iliyoasisiwa miaka ya 1930 na Wittgenstein na kuiendeleza zaidi katika taaluma ya isimu mwaka (1953). Nadharia hii inasisitiza kueleza maana kwa kuzingatia matumizi ya maneno. Nadharia ya Maana ni Matumizi ilichaguliwa kuchambulia semi kwa kuwa inazingatia muktadha wa matumizi wa neno linalohusika katika kueleza maana. Hii ni kwa sababu maana ya semi haipatikani kwa kuangalia neno mojamoja linalounda semi hiyo bali huzingatia muktadha wa matumizi ya neno hilo na uhusiano kati ya neno moja na jingine. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba ingawa semi ni kipengele muhimu katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, kipengele hiki hakijafanyiwa kazi ipasavyo na hivyo kinakabiliwa na upungufu mkubwa. Miongoni mwa upungufu unaokikabili kipengele cha uingizaji wa semi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu ni kukosekana kwa kanuni maalumu ya kuingiza semi na semi nyingi kutofafanuliwa wala kutolewa maelezo ya kina. Katika utafiti huu inapendekezwa kwamba kuna umuhimu wa kuwa na kanuni maalumu ya kuingiza semi katika kamusi na kwamba semi zote zilizoingizwa katika kamusi ni vema zikafafanuliwa ili kuwasaidia watumiaji wa kamusi kuzielewa vema.

About Library

The University of Dar es Salaam Library is a vital source of scholarly information that facilitates users to get access to learning and research resources during their studies. It provides access to a wide range of resources in both print and digital formats and conducive reading environment for users, regardless of their physical conditions. All registered users are eligible to access library resources and can borrow print materials from general shelves for a specific period of time.

Useful Links

Koha Staff Login

University Research Repository

WebMail

Aris

Book Study Room

Mara Oral History

Hansard

SOCIAL MEDIA

Instagram

Facebook

Twitter

YouTube

WhatsApp

Ask Librarian

Contact Us

Postal Address
P.O.Box 35092
Dar es Salaam

Call Us: +255 22 2410500/9 Ext. 2165 ; Direct line +255 22 2410241

Fax No:: +255 22 2410241

Email:: directorlibrary@udsm.ac.tz

2025 University of Dar es Salaam - University Of Dar Es Salaam Library
Term of use / Privacy Policy